Jumanne, 30 Januari 2018

Jumatatu, 29 Januari 2018

MATOKEO: CONGO, KOMBE LA WAMACHINGA LA MPIRA WA MIGUU, BINGWA NI MIMI

*Gazeti La Wamachinga - WASPOC HABARI*

Na *M. M. Jumanne*

Hayo ni maneno ya Meneja wa moja ya timu ya *Wamachinga Sports Club Tanzania - WASPOC* ya mtaa wa *CONGO* yenye namba ya usajili *WASPOC-T-02* huyasema kila amalizapo mechi zake kwa ushindi mnono kuwa *_"KOMBE HILI LA WAMACHINGA 2018 NI LAKE, MABINGWA NI WAO"_*. Husema timu yake imejipanga kwa kila idara vya kutosha kuonesha ubabe kwa timu za kundi B ambazo timu mbili bado hajacheza nazo na mbili alishacheza nazo bali zile za kundi lake ameshacheza nazo zote na ameshazifunga timu tatu zote, kama ifuatavyo:-.
CONGO 3⃣ - 1⃣ SIMA
MUHONDA 0⃣ - 5⃣ CONGO
AGREY 1⃣ - 2⃣ CONGO.

Na za kundi B:
MCHIKICHI 2⃣ - 1⃣ CONGO
CONGO 1⃣ - 1⃣ NYAMWEZI CHINI
CONGO 2⃣ - 5⃣ MCHIKICHI, bado NYAMWEZI JUU NA TANDAMTI tu.

Vilevile, Meneja alisema kwa kumalizia *TUKUTANE KOMBENI* Jumamosi hii kwenye Mechi yake ya ufunguzi, wadau na wapenzi wa soka mje kwa wingi mno: *SIMA 🆚 CONGO*

*_MATOKEO YA JANA_*

Mechi: *AGREY 1⃣ - 2⃣ CONGO*
Shindano: *Mechi ya Ndani ya Kirafiki - Maandalizi ya Kombe la WAMACHINGA la Mpira wa Miguu*.
Siku: *JUMATATU*
Tarehe: *JANUARI 29, 2018*
Muda: *Saa 10:00 JIONI*
Uwanja : *BENJAMIN WILLIAM MKAPA*
Kiingilio: *HAKUNA*

*#WASPOC #KAZIKAZI*

Jumapili, 28 Januari 2018

MATOKEO: NYAMWEZI CHINI ACHANA MKEKA LEO

*Gazeti La Wamachinga - WASPOC HABARI*

Na *M. M. Jumanne*

Moja ya Timu ya *Wamachinga Sports Club Tanzania - WASPOC* ya mtaa wa *NYAMWEZI CHINI* yenye namba ya usajili *WASPOC-T-05* kutoka Shina la kwanza la Klabu la WASPOC liitwalo *BIN AFFAN & SONS CO. LTD* leo imechana mkeka kwa kufungwa na kikosi cha timu ya *NDOLA FC* kwenye mechi ya kirafiki ya nje.

Mpaka sasa *NYAMWEZI CHINI* imeshacheza mechi 2 za nje za KIRAFIKI (Kashinda 1 na Kafungwa 1) na za ndani ni 2 tu.

MATOKEO: *NDOLA FC 2⃣ - 0⃣ NYAMWEZI CHINI*

Shindano: *MECHI YA NJE YA KIRAFIKI*.
Siku: *JUMAPILI*
Tarehe: *JANUARI 28, 2018*
Muda: *Saa 8:30 MCHANA*
Uwanja: *JAKAYA M. KIKWETE YOUTH PARK*
Kiingilio: *HAKUNA*

TUKUTANE TENA KESHO.

Mechi: *AGREY 🆚 CONGO*
Shindano: *Mechi ya Ndani ya Kirafiki - Maandalizi ya Kombe la WAMACHINGA la Mpira wa Miguu*.
Siku: *JUMATATU*
Tarehe: *JANUARI 29, 2018*
Muda: *Saa 10:00 JIONI*
Uwanja : *BENJAMIN WILLIAM MKAPA*

*#WASPOC #KAZIKAZI*

MATOKEO: MUHONDA NA SIMA NI X KWENYE NORMAL

Mchezo uliochezwa jana uwanja wa Benjamin W. Mkapa saa 10:00 Jioni ambao umewakutanisha timu mbili zilizosajiliwa kushiriki kwenye Kombe la WAMACHINGA la Mpira wa Miguu kati ya MUHONDA na SIMA walifungana moja moja.

Jumamosi, 27 Januari 2018

MECHI: NDOLA 🆚 NYAMWEZI CHINI (SHINA LA WASPOC LA KWANZA LA BIN AFFAN & SONS CO. LTD - KARIAKOO)

Usikose kesho kuja kuangalia mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na KOMBE LA WAMACHINGA LA MPIRA WA MIGUU, mechi ya nje.


MECHI: NYAMWEZI CHINI ITAMTOBOA MACHO, MACHO KODO?

Moja ya Timu ya Wamachinga Sports Club Tanzania - WASPOC ya mtaa wa NYAMWEZI CHINI kutoka Shina la BIN AFFAN & SONS CO. LTD la Tawi la Soko kuu la Kariakoo la WASPOC imejiandaa vya kutosha kukabiliana na kikosi cha timu ya MACHO KODO hapo kesho kiwanja cha Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park.

Jumamosi, 20 Januari 2018

MATOKEO: CONGO YAKAZA KAMBA KWA AZANIA

Gazeti La Wamachinga - WASPOC HABARI

Timu ya *Wamachinga Sports Club Tanzania* ya mtaa wa CONGO yenye namba ya usajili WASPOC-T-02 leo imechuana vyema na timu ya AZANIA kwenye marudiano, ambapo awali CONGO walikuwa wageni wa AZANIA na kufungwa katika mchezo huo uliopita. Mpaka sasa CONGO ameshacheza mechi 3 za nje za kirafiki kuliko timu yoyote ya WASPOC.

Shindano: *MECHI YA NJE YA KIRAFIKI*.
Siku: *JUMAMOSI*
Tarehe: *JANUARI 20, 2018*
Muda: *Saa 10:00 JIONI*
Uwanja: *BENJAMIN WILLIAM MKAPA*
Kiingilio: *HAKUNA*

CONGO 2⃣ - 2⃣ AZANIA

WAFUNGAJI
CONGO
Goli 1 - Hamisi Mohammed 7' Kipindi cha I
Goli 1 - Yusuph Musa 31' Kipindi cha II (NYOTA WA MCHEZO) 

AZANIA
Goli 1 - 9' Kipindi cha II
Goli 1 - 38 Kipindi cha II

TUKUTANE TENA MAANDALIZINI.

#WASPOC #KAZIKAZI