Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Wamachinga Tanzania (WASPOC) na Rais wa Tanzania Freestyle Football Association - #TFFA (Chama cha Uchezeaji wa Mpira wa Miguu Tanzania) ndugu Morison Mosses Jumanne alimtembelea Mhe. Harrison Mwakyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye Ofisi ndogo ya Wizara iliyopo Dar Es Salaam uwanja wa Taifa.
Ndugu Mwenyekiti aliongea mengi na Waziri kuhusu Michezo yote anayoisimamia kama Mtawala katika Vyama na Vilabu vya michezo kama vile Freestyle Football, Neymar Jr's Five, Panna, Teqball na FootPool ambayo michezo hii yote inakuwa rahisi kwake kuitekeleza kupitia Klabu ya Wamachinga Sports Club Tanzania ijapokuwa kwa sasa klabu imejikita katika soka lakini mbeleni itashughulika na Michezo hiyo ili kuleta Mapinduzi na Maendeleo katika vilabu vingine vinavyoshughulika na mchezo mmoja wakati vilabu hivyo vina usajili wa klabu ya Michezo (Sports Club).
WASPOC KAZI KAZI
WASPOC
Klabu Ya Mapinduzi, Klabu Ya Maendeleo.
ILITOLEWA NA: Gazeti la WAMACHINGA
HABARI ZA: Michezo
TAREHE: Julai 2, 2018 Jumatatu.